Zaidi ya watoto 600 wapata Kipaimara Parokia ya Nyabula

Zaidi ya watoto 600 kutoka katika vigango saba (22) vya Parokia ya Nyabula Jimbo Katoliki la Iringa wamepatiwa kipaimara toka kanda tatu: IHIMBO, MAGULILWA NA NYABULA.

Kanda ya Ihimbo ina vigango nane (8) na waimarishwa mia moja sitini na moja (161) idadi ya maketekista kumi na tatu (13), idadi ya JNNK thelathini nan ne (34) na viongozi wa Halmashauri ya Walei thelathini na tisa (39). Katika kanda kuna makanisa manne (4) yaliyo kamilika, makanisa mawili (2) yenye uhitaji wa mareekebisho na makanisa mawili (2) ambayo ujenzi unaendelea.

Kanisa la Ihimbo
Kanisa la Magulilwa

Kanda ya Magulilwa ina vigango sita (6) na waimarishwa mia moja sitini na nne (164) idadi ya maketekista kumi na tano (15) idadi ya JNNK thelathini na tano (35) na viongozi wa Halmashauri ya Walei thelathini (30). Katika kanda kuna makanisa sita (6) yaliyo kamilika.

Kanisa la Nyabula

Kanda ya Nyabula ina vigango nane (8) na waimarishwa mia tatu thelathini na nane (338) idadi ya maketekista kumi na tisa (19) idadi ya JNNK hamsini na sita (56) na viongozi wa Halmashauri ya Walei arobai (40). Katika kanda kuna makanisa saba (7) yaliyo kamilika na kanisa moja (1) ambalo ujenzi unaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *