LOGO NYABULA PARISH Transparent

Karibu Parokia ya Nyabula.

Pd. Emil I. Kindole 
 PAROKO NYABULA

Parokia ilianzishwa mwaka 1932 na Mmisionari wa Bikira Maria Konsolata Padre Emilio Ogge na huyo ndiye Paroko wa kwanza wa eneo hili. Padre Emilio alifuatiwa na P. Carlo Viglieti mwaka 1934 -1950 ambapo Padre Viglieti alitumwa mwaka 1956 kuanzisha Parokia ya Usokami.

Baadae alifuata Padre Natale M. Eusebio mwaka 1951 – 18/8/1959 na ndiye mjenzi wa kanisa kubwa lililopo. Siku alipokwenda Tosamaganga kumwita Askofu Betramino kuja kubariki kanisa, alifariki huko ghafla na mwili wake kurudishwa hapa na kuzokwa nyuma ya Kanisa. Baadae walifuata maparoko Egidio Crema 1959 – 1966, Padre Romano Ceschia 1956 – 1975, Padre Joseph Morati 1975 – 1982, Padre Scacia 1982 – 1986, Padre Mario Baseggio 1986 – 1996, Padre Cornelio Dalzocchio 2000 – 2003, Padre Peter Lumiri 2003 – 2005. Na tangu Novemba 2005, Parokia imekabidhiwa kwa Mapadre wa Jimbo. Padre Benjamini Mfaume Paroko, na Padre Joy Ashock. Baadae wamefuata Padre Emily Kindole, Padre Protas Chelula, Padre Laetus Mbegasi, Padre Justin Msosi, Padre Stanslaus Mhumbila, Padre Eugen Ngatunga na Padre Marco Kihwelo. Hakika Parokia hii imekuwa hivi kwa sababu ya wamisionari wetu wa Bikira Maria Konsolata, wakiwepo maparoko na wasaidizi wao kama Padre Joseph Pochettino, Michael Rosin, Silvio Trucchi, John Medri, Angelo Pizzaia, Mario Natalini, Angelo Parola, Daniel Ruiz, Angelo Pagani, Drago Bevanda, Alessandro di Martino, Piero Clavero, Emilio Chiuchi, Mario Biestra, Michael Njagi, Clement Balufuti, Elias Mugo, Israel Amador Avila na Stanley Muriuki. Tunawashukuru mapadre, hawa maaskofu na wakuu wao kwa shughuli nzito waliyoifanya kwa ajili ya kutangaza Neno la Mungu katika eneo hili. Walio hai tunawaombea Baraka za Mwenyezi Mungu na waliotangulia katika makao ya milele wapumzike kwa Amani. Amina.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kila kigango bofya jina la kigango husika, mkono wa kushoto.

Miradi ya Parokia

ujenzi wa shule

Elimu

Uamuzi huu unatokana na makubaliano kuwa shule ya St. Thomas Nyabula Pre and Primary  zaidi ya elimu ya kawaida, itatoa malezi ya kikristo yanayolenga kumlea mtu katika ukamilifu wake; ili awe mtu bora alifae Taifa.

Malulumo church

Jumuiya ya Kikatoliki ya Malulumo iliona umuhimu wa kuwa na mahali pa kukusanyika ili kusherehekea imani yao tangu mwaka 2011.

kipaimara 2021

Zaidi ya watoto 600 wapata Kipaimara Parokia ya Nyabula

Mheshimiwa Fr. Vicent Mwagala, V.G kuwapatia waimarishwa mia sita sitini na tatu (663) toka kanda tatu: IHIMBO, MAGULILWA NA NYABULA.

Zaburi 4:1

Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Umenifanyizia nafasi wakati wa shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu.